|
Taifa Stars |
Na Boniface Wambura,
Addis Ababa
TIMU ya soka
ya ya taifa ya Tanzania, imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia
uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mechi hiyo
iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana
na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza
kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua sita
kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa
wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao
hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki mmoja
wa Ethiopia.
Bao la
ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji
Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi
uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.
Taifa Stars
inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya
Ethiopian Airlines.
Taifa Stars:
Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri
Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi
Kazimoto na Mbwana Samata.