KWA HABARI ZILIZO HARIRIWA NA KUHAKIKIWA NA WACHAMBUZI MAKINI USIKOSE KUTEMBELEA HAPA KILA SIKU
Friday, June 22, 2012
Wednesday, June 20, 2012
MKUTANO WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA NA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR
Baadhi ya Wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba wakiwa katika Mkutano wa Tume hio na Waandishi wa Habari uliofanyika Bwawani Mjini Zanzibar. |
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika Bwawani Mjini Zanzibar. |
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika Bwawani Mjini Zanzibar. |
Mwandishi wa Habari Kutoka Gaazeti la Majira Mwajuma Juma akiuliza
maswali katika Mkutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika
Bwawani Mjini Zanzibar.
|
Mwandishi wa Habari Kutoka Idara ya Habari Maelezo akiuliza maswali katika Mkutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika Bwawani Mjini Zanzibar. |
WATANZANIA WATAKIWA KUJIPANGA KUHAMA KUTOKA ANALOJIA KUJA DIGITALI
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA
Waanzania wametakiwa kujiandaa kuhama katika mfumo wa mabadiliko ya
anaelojia kwenda katika mfumo wa digital ambao hadi ifikapo Desemba
31 mwaka huu matangazo ya anaelojia yatazimwa rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa mkurugenzi mkuu wa
mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Frederick Ntobi amesema kuwa
kuanzia januari 2013 wananchi hawataweza tena kutumia mfumo uliopo wa
sasa wa anaelojia.
Amesema kuwa ili kwenda na utandawazi uliopo hadi ifikapo januari 2013
dunia nzima itakuwa imehama katika mfumo wa kutumia anaelojia katika
luninga zao hivyo ni vema wananchi wakaanza kujipanga mapema ili
kuhakikisha kuwa kila mtu anafikiwa na huduma hiyo.
Amengeza kusema ku wa ili mfumo huoi ukamilike ni vema jamii
ikahakikisha kuwa lazima inakuwa na kifaa kiitwacho kingamuzi ambacho
ndicho kinatumika katika kubadilisha mfumo ili kuweza
kufanikiwa
katika ubadilishaji huo.
Bw ntobi ametaja faidsa ya kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja kuwa na
matumizi bora ya masafa ,kupata huduma bora za ziada mfano kulipia
bili ya umeme,kutuma pesa pamoja na kupata intenet pindi uwapo kwenye
luininga zao
Pia alitaja faida ingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajira kwa
kuwa mfumo utachangia kuongezeka kwa makampuni nmengi ya utangazaji.
OMOTOLA kuizindua Super Star ya Wema Jumapili Giraffe Hotel
.Ni onyesho maalum la familia
MKALI
wa filamu nchini Nigeria na Afrika, Omotola Jalade atazindua filamu ya
Wema Sepetu Jumapili hii katika Ukumbi wa Hoteli ya Girafee Ocean View,
iliyopo Mbezi Beach.
Filamu
hiyo iitwayo Super Star imechezwa na Wema, ikionyesha maisha ya mtu
maarufu na changamoto anazozipata ikiwemo kuandikwa mambo mbalimbali
ikiwemo taarifa za vyombo vya habari.
Katika
uzinduzi huo, bendi kutoka Tanzania House Of Talent (THT) watatoa
burudani, kabla ya mashabiki kupata nafasi ya kupiga picha na msanii
huyo.
Omotola,
ambaye ni mke wa rubani Kapteni Matthew Ekeinde, ambao walifunga ndoa
yao angani kwenye ndege atatoa nafasi ya kupiga picha na watu kadhaa.
Katika uzinduzi huo, pamoja na burudani ya muziki, mashabiki watakaofika hapo, watapata pia fursa ya kuiona filamu ya Super Star katika viwanja hivyo vya hoteli hiyo iliyoko ufukweni.
Omotola ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki.
Msanii
huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza filamu kutokana
na kuandikwa vibaya, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye uzinduzi
huo ambao kiingilio kitakuwa Sh 30, 000 kwa wakubwa na watoto 10,000.
MTOTO WA MR BLUE AITWA HERRY JINA LA BABA NA MTOTO WA DOGO HAMIDU ANAITWA HERRY.
Drama
Boy Herry Sameer Rajab muite Mr Blue Jumapili iliyopita amebahatika
kupata mtoto wa kiume kutoka kwa his long time girlfriend Wahida, Hivi
karibuni pia Dogo Hamidu/Nyandu Toz nae alipata mtoto wa kiume akampa
jina la mshikaji wake yani Herry (Mr Blue). Hii ikiwa ni kushow love kwa
Mr Blue na fans.Mtoto wa Mr Blue amempa jina lake la Herry a.k.a Nyandu Toz. Mr Blue ni baba Herry na Nyandu Toz ni baba Herry..Safi.
Sunday, June 17, 2012
KILA LA HERI TAIFA STARS LEO NA MSUMBIJI
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo jioni wanateremka dimbani huko msumbiji kumenyana na Wenyeji wao Msumbiji katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza michuano ya Africon
Kocha Mkuu wa Taifa stars Kim Poulsen amesema kikosi chake kiko katika hali nzuri hii leo kuweza kuwawakilisha vema watanzania huko msumbiji
Ikumbukwe Katika Mchezo wa awali uliopigwa Hapa nyumbani katika uwanja wa Taifa Timu hizo zilitoshana nguvu kwa kwenda sare ya bao 1-1 na hivo mechi ya leo ikiwa ni muhimu kwa kila timu ili ijiweke katika mazingira mazuri ya kufuzu Katika Fainali hizo za Africon
Blog hii inaungana na watanzania wote kuiombe Taifa Stars leo ili iweze kuibuka na ushindi huko msumbiji
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI TAIFA STARS
Friday, June 15, 2012
TANZANIA LEO KUUNGANA NA MATAIFA MENGINE KUADHIMISHS SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
UTANGULIZI:
Mwaka 1990, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) ulipitisha Azimio la nchi 51 za wanachama wa Umoja huo kuhusu kukumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto kilichopo Afrika ya Kusini ambao waliuawa kinyama na iliyokuwa Serikali ya Makaburu ya nchi hiyo tarehe 16 Juni, 1976.
Watoto hao walikuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za kibinadamu
MADHUMUNI:
Pamoja na kukumbuka mauaji hayo ya kinyama, madhumuni mengine ya kuadhimisha siku hiyo ni pamoja na yafuatayo: kuwa na fursa ya kusisitiza wajibu wa Serikali za Afrika kwa watoto; kuziwezesha Serikali hizo kuandaa na kutekeleza mipango ya taifa ya kuwaendeleza watoto; Kuinua kiwango cha uelewa na ufahamu wa matatizo yanayowakabili watoto wa Afrika.
Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo mwanachama wa Umoja wa Afrika, imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku hii kwa miaka kumi na saba (17) mfululizo tangu mwaka 1991. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hutumia siku hii kutafakari kwa kina matatizo mbalimbali yanayowakabili watoto na vile vile kutafuta namna ya kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo.
Serikali inapata pia wakati mzuri wa kutangaza sera, programu na mipango mbalimbali inayohusu masuala ya watoto na kuhamasisha jamii kuchangia kuondoa matatizo mbalimbali ya watoto kote nchini.
Kwa upande mwingine, maadhimisho haya ni sehemu ya utekelezaji wa sera zetu zinazohusu kuwaendeleza watoto, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu haki na ustawi wa watoto.
KAULI MBIU:
haki za watoto wenye ulemavu ni wajibu wetu kuzilinda ,kuziheshimu,kuziendeleza na kuzitimiza
Kaulimbiu hii inatukumbusha kuwa kuna haja ya kuliangalia upya tatizo la ongezeko la watoto wanaoishi mitaani kutokana na hali halisi ya tatizo hili linavyoonekana hapa nchini..
SHUGHULI ZITAKAZOFANYIKA:
Maadhimisho haya huambatana na shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo hufanyika kitaifa na kimkoa. Mwaka huu hapatakuwepo na maadhimisho kitaifa, bali kila mkoa utapata fursa ya kupanga namna ya kuadhimisha siku hii kulingana na rasilimali zilizopo mkoani, wilayani na vijijini.
MWISHO:
Ni matarajio ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuwa vyombo vya habari vitatoa ushirikiano wa hali ya juu katika kuhamasisha jamii yetu juu ya umuhimu wa Siku hiyo.
Vile vile, Wizara inapenda kutumia fursa hii kuikumbusha mikoa kuhakikisha kuwa siku hiyo inaadhimishwa katika maeneo yao na kwa kutumia rasilimali walizo nazo.
Mwisho, ninapenda kuchukua tena fursa hii kuwakumbusha Watanzania wote na viongozi wetu hapa nchini kuwa watoto ni taifa la leo na la kesho, hivyo wanapaswa kuendelezwa, kulindwa, kushirikishwa, kuishi na kutokubaguliwa Nawatakia kila la kheri katika kufanikisha maadhimisho haya.
WATOTO NI TAIFA LA LEO NA KESHO.
Dkt. Bilal azindua Mradi wa Kuinua Ubora wa Elimu ya Msingi mkoani Mtwara
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata
utepe, kuzindua Mradi wa Kuinua Elimu ya Msingi ijulikanayo kama 'Tz 21
Century Basic Education Program, mradi uliofadhiliwa na Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID). Kulia ni Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amezindua
Mradi wa Kuinua Ubora wa Elimu ya Msingi wa “TZ 21st Century Basic
Education Program”
Sherehe za uzinduzi wa
mradi huo ambao unalenga kuinua ubora ya elimu ya msingi kwa kutumia
teknolojia ya habari na mawasiliano umeanzishwa na Shirika la Kimataifa
la Maendeleo la Marekani (USAID) zimefanyika leo katika shule ya msingi
Kambarage mkoani Mtwara.
Akihutubia katika
uzinduzi huo Dk. Bilal aliwataka Watanzania kuendelea kujenga
imani na mfumo wa elimu uliopo nchini kwani ni mfumo bora ukilinganisha
na mifumo ya elimu iliyopo katika nchi nyingine za Kusini Mashariki mwa
Afrika.
Makamu wa Rais alisema kwa muda mrefu
sasa, imani imejengeka katika jamii kwamba elimu inayotolewa hapa nchini
ni duni na inahitaji kubadilishwa.
Aliwahakikishia
Watanzania kuwa elimu inayotolewa hapa nchini haijashuka kiasi hicho
kwani matokeo ya Utafiti wa Kufuatilia Ubora wa Elimu katika nchi za
Kusini Mashariki mwa Afrika (SACMEQ) ya mwaka 2000 na 2007 yanaonyesha
kuwa ukilinganisha na nchi nyingine, mfumo wa elimu hapa nchini ni bora.
“Kwa
mfano, kati ya nchi 15 zilizofanya utafiti huo, nchi yetu ilifanya
vizuri katika somo la Hisabati na Kusoma na kuwa kati ya nchi bora za
kwanza katika utafiti wa mwaka 2007,” alidokeza Dkt. Bilal.
Makamu wa Rais pamoja na kukiri kwamba kuna watoto wachache wanaomaliza darasa la saba bila ya kuwa na stadi za kusoma na kuandika vizuri lakini alisema wapo wengi wanaomaliza na kufanya vizuri na kuwasihi wananchi wasikatishwe tamaa na maoni ya watu mbalimbali kuhusu kushuka kwa elimu nchini bali waongeze juhudi na kuwa na fikra chanya katika kutoa elimu bora.
Dkt. Bilal alitumia fursa hiyo pia kuwataka wadau wa elimu kulipa umuhimu wa pekee suala la upimaji na utahini katika shule za msingi kwani mitihani bora bado ni changamoto ambayo inahitaji kuangaliwa upya na wazazi na walimu kwa upande wao wana jukumu la kuhakikisha watoto wanasoma maana elimu bora ya msingi ndiyo itakayosaidia kuondokana na umaskini na kuwa na maendeleo endelevu.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa alisema mradi huo utasaidia katika kufanikisha utekelezaji wa MMEM Awamu ya III (2012-2016) hususan katika kuinua kiwango cha ubora wa elimu ya msingi itolewayo nchini.
Naye Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt alielezea kufurahishwa kwake kwa kuingizwa mradi huo katika utaratibu wa kutoa taarifa za elimu (Education Management Information System) akiwa na matumaini kwamba utasimamiwa na kuendelezwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
SERIKALI YA TANZANIA YASAINI MKATABA NA BENKI YA DUNIA KUHUSU MPANGO WA TASAF (3
Katibu mkuu wizara ya fedha Ndg.Ramadhani Kijah kushoto na Mwakilishi wa Benki ya dunia Pilppe Dongier wakikabidhiana mikataba baada ya kumaliza kusaini |
Thursday, June 14, 2012
TUZO ZA TASWA ZILIVYOFANA DIAMOND JUBILEE
Rais wa TFF, Leodegar Tenga wa pili kulia akiwa na Jellah Mtagwa kushoto kwake |
Familia ya ndondi |
Wadau wa ndondi |
Tedi Mapunda kulia na bosi wake |
Eiphraim Mafuru kulia |
Maswahiba wa siku nyingi, Shaaban Mkongwe kulia akiwa Waziri Mahadhi |
Beki wa Mtibwa Salum Swedi 'Kussi' |
Kaburu kulia akikabidhi tuzo |
Daud Salum 'Bruce Lee' kulia akikabidhi tuzo |
Athumani Hamisi akikabidhi tuzo |
Asha Baraka akikabidhi tuzo |
Mafuru akikabidhi tuzo |
Ridhiwani Kikwete kulia akiwa na Benny Kisaka kushoto, cheko la maana |
Dioniz Malinzi kushoto akikabidhi tuzo |
Kapombe akipokea tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi |
Mzee Matumla akimkabidhi Kaburu tuzo ya Emmanuel Okwi |
Mwenyekiti wa RT, akimkabidhi tuzo Mwanahamisi Gaucho |
Aggrey Morris kushoto akipokea tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka |
Ally Choky akikabidhi tuzo |
Mafuru akipakia msosi |
Kim Poulsen kulia akiwa na nani sijui |
Jamal Rwambow kulia na Kaburu wakati wa maakuli |
Serengeti Beer inapokolea, mambo huwa hivi... |
Mzee El Maamry akimkabidhi tuzo George Tarimo |
Mzee Mwinyi akimkabidhi tuzo Adolph Rishard |
Mzee Mwinyi akimkabidhi tuzo Peter Tino |
Mzee Mwinyi akikabidhi tuzo |
Waziri Mahadhi akimpokelea tuzo marehemu baba yake, Omar Mahadhi |
Kaburu akimsaidia Kapombe kupokea tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka 2011 |
Juma Pinto akikabidhi tuzo |
Zena Chande na swahiba zake |
Shaffih Dauda kulia, Amour Hassan na Michael Maluwe |
Tullo Chambo na bosi wake |
MAJINA YA WASHINDI
1: OLIMPIKI MAALUM-Zanzibar
Ahmada Bakar:
2:OLIMPIKI MAALUM-TANZANIA BARA
HERITH SULEIMAN
3: PARALIMPIKI: WANAUME
ZAHARANI MWENEMTI
4:PARALIMPIKI: WANAWAKE
FAUDHIA CHAFUMBWE
5: KIKAPU: WANAUME
GEORGE TARIMO:
6: KIKAPU WANAWAKE
EVODIA KAZINJA:-
7: NETIBOLI:
LILIAN SYLIDION
8: GOFU WANAWAKE:
MADINA IDDI
9: GOFU WANAUME:
Frank Roman:
10: NGUMI ZA RIDHAA
SULEIMAN SALUM KIDUNDA
12: WAOGELEAJI MWANAMKE
MAGDALENA MOSHI
WAOGELEAJI MWANAUME
AMMAAR GHADIYALI - MEN
13:JUDO...
AZZAN HUSSEIN KHAMIS (ZANZIBAR)
14:JUDO BARA: . MBAROUK SELEMANI
14: WAVU WANAWAKE
THERESIA ABWAO
15: WAVU WANAUME
MBWANA ALLY
16: NGUMI ZA KULIPWA
Nasibu Ramadhan
17. TENISI:Wanaume
WAZIRI SALUMU
18. TENISI WANAWAKE:
REHEMA ATHUMANI
20: BAISKELI (Wanawake)
Sophia Hussein
-
21: BAISKELI WANAUME
Richard Laizer
22: WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE
Mbwana Samatta-
23: MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI
SHOMARI KAPOMBE- (soka) SIMBA
24: MCHEZAJI WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA
Emmanuel Okwi-Simba
25: SOKA (WANAWAKE)
MWANAHAMISI OMARI
26: SOKA WANAUME
Aggrey Morris-Azam:
27: RIADHA
WANAWAKE
Zakia Mrisho:
28: RIADHA WANAUME
Alphonce Felix:
29: MIKONO WANAUME
Kazad Monga-Magereza Kiwira
Faraji Shaibu Khamis-Nyuki Zbar
30: MIKONO WANAWAKE
Zakia Seif-Ngome Dar
31: Kriketi WANAWAKE
Miss. Monika Pascal
32; KRIKETI WANAUME
Mr. Kassimu Nassoro
33: TUZO YA HESHIMA:
KIKOSI KILICHOFUZU FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA 1980
34:MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011-
SHOMARI KAPOMBE
Subscribe to:
Posts (Atom)